Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe.Kanali Ahmed Abbas Ahmed amesema Serikali itaendelea kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kutambua na kuthamini mchango wao katika ukuaji wa Uchumi
Amesema katika fedha zinazotolewa na Halmashauri kwa makundi maalum ya Vijana, Wanawake na watu wenye Ulemavu ambapo mwaka wa fedha 2021/2022 na Disemba 2022/2023 Halmashauri za Mkoa wa Mtwara kutokana na fedha za mapato ya ndani zimekopesha kiasi cha shilingi Bil 3.3 kwa vikundi 632 vikiwemo vya wanawake
RC amesema katika fedha hizo shilingi Bil 1.7 zimetokana na makusanyo ya makundi husika,shilingi Bil 1.6 zimetokana na marejesho ,Shilingi Bil 1.6 zimekopeshwa kwa vikundi 356 vya wanawake na vijana,Shilingi Bil.1.3 vikundi 177 vya watu wenye ulemavu na shilingi Mil 345 kwa vikundi 145
Aidha kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Halmashauri za Mkoa wa Mtwara zimeweka makadirio ya kukopesha kiasi cha shilingi Bil.2.4 kwa ajili ya mikopo ya vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu ambapo ametoa wito kurejesha mikopo hiyo kwa wakati sambamba na wanawake kuchangamkia fursa hiyo ili kujikwamua kiuchumi
Amesema hayo Machi 8,2023 katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yenye kauli mbiu “Ubunifu na Mabadiliko ya Teknolojia chachu katika kuleta Usawa wa Kijinsia” ambapo Kimkoa yamefanyika katika viwanja vya shule ya msingi Amani Halmasahauri ya Wilaya yaTandahimba na kutaka jamii kutathimini na kutafakari kwa pamoja jinsi Mkoa ulivyopiga hatua
“Nachukua fursa hii kuhimiza wewe mjasiriamali kujenga hamasa binafsi ya kujifunza maarifa mapya yatakayokusaidia kuwa mbunifu katika biashara yako,nawapongeza wanawake wajasiriamali ambao mmejitokeza kuonesha bidhaa zenu ,taasisi zote na wananchi mlioshiriki katika siku hii ya wanawake ambayo imefana sana,”amesema RC
Kwa upande wa viongozi mbalimbali waliopata nafasi ya kuzungumza wamesistiza wanawake kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na kutoa taarifa za ukatili unaofanyika katika jamii ili vyombo husika viweze kuchukua hatua za kisheria kwa wahusika
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa