Na Kitengo cha Mawasiliano.
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amewaagiza Viongozi ngazi ya Kata na kufanya Oparesheni maalumu kutafuta watoto ambao hawajaripoti kuanza Masomo kwa kigezo Cha kutokua na sare za Shule.
DC Sawala ameyasema ayo Leo Januari 15, 2024 alipotembelea Shule ya Msingi Litehu kuona Madarasa yaliyoezuliwa kutokana na Mvua kubwa iliyonyesha na kusababisha Vyumba viwili vya Madarasa Kubomoka.
DC Sawala amesisitiza wazazi kuwapeleka watoto wao ili wapate haki yao ya kupata Elimu kwa kuwa tayari Serikali imejenga Miundombinu Bora ya Madarasa na kuongeza kuwa Wazazi watakaokiuka hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa