Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe.Kanali Ahmed Abbas amezindua msimu wa pili wa Korosho Marathon mwaka 2023 katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba
Uzinduzi huo umefanyika Mei 13,2023 ambapo wananchi wamejitokeza kushiriki mbio fupi za Km 5 ambazo zilianzia Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri
Rc ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki mbio za Korosho Marathon msimu wa pili ambazo zitafanyika rasmi Septemba 2,2023 katika uwanja wa Nangwanda Sijaona uliopo Manispaa ya Mtwara Mikindani ambapo washiriki watajisajili na kukimbia Km 5,Km 10 na Km 21
"Riadha ni furaha,riadha ni umoja,riadha ni amani na riadha ni afya ,nawapongeza wananchi kwa kujitokeza kwa wingi lakini pia mjitokeze kwa wingi kushiriki Mbio za Korosho Marathoni msimu wa pili Septemba 2,2023," amesema RC
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa