Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe.Kanali Ahmed Abbas Ahmed ametoa wito kwa wanunuzi wa korosho kununua kwa bei inayoridhisha ili kumtia moyo mkulima wa zao la Korosho
Amesema hayo Oktoba 21,2022 wakati akifungua Mnada wa kwanza wa Korosho ulioendeshwa na Chama Kikuu cha Ushirika Tanecu ambao umefanyika katika ghala la kijiji cha Mitondi B Kata ya Kitama Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba
"Serikali itaendelea kudhibiti ubora wa korosho ili kuendelea kuipa thamani Korosho ya Tanzania lakini wanunuzi mnunue bei nzuri ili wakulima wasivunjike moyo kwa kuzingatia kuwa kipindi hiki cha mauzo ni muhimu kwa Wakulima wa Korosho,"amesema Rc
Makampuni 15 yameshiriki katika mnada huo wa stakabadhi ghalani ambapo Jumla ya Korosho zilizopo katika maghala manne ya Tanecu ni Tani 1610 huku Tandahimba ikiwa na Tani 1122 kati ya tani 1610
Katika mnada huo Korosho zote bei ya juu ilikuwa ni shilingi 2011 (Elfu mbili na kumi na moja) bei ya chini ni shilingi 1630 (Elfu moja mia sita na thelathini) ambapo wakulima wameahirisha kuuza korosho zao kwa bei hiyo
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa