Na Kitengo cha Mawasiliano.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Kanali Ahmed Abbas leo Desemba 20, 2023 ametembelea na kukagua Maendeleo ya Ujenzi wa Shule ya Sekondari Mahuta na Shule ya Msingi Mambamba na kuwapongeza viongozi kwa usimamizi Mzuri huku akiwataka Wananchi kutumia fursa hiyo kuwahimiza wanafunzi kwenda Shule mara baada ya Shule hizo Mpya Kufunguliwa.
"Uwezekano wa kuwaleta wanafunzi mwakani upo, hivyo nitoe Rai kwa Wazazi kuhakikisha wanawaleta wanafunzi ili miundombinu hii ikalete maana iliyokusudiwa" Kanal Abbas
Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuendelea kuleta Miradi yenye tija kwa Wananchi wa Tandahimba.
Kwa Upande wao Wananchi wa Mahuta na Mambamba wametuma salamu za kumshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali watoto wao kwa kuboresha Miundombinu ya Elimu.
Ujenzi wa Shule ya Sekondari Makondeni iliyopo Kata ya Mahuta umegharimu Tsh.Milioni 560.6 fedha kutoka Serikali kuu kupitia Mradi wa SEQUIP sambamba na Shule ya Msingi Mambamba inayogharimu Tsh.Milioni 331.6 ikiwa ni fedha kutoka Serikali kuu kupitia Mradi wa BOOST inatarajiwa kuanza kutumika ifikapo Januari 2024 .
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa