Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe.Kanali Ahmed Abbas Ahmed amekabidhi mabati 200 na msaruji mifuko 20 kwa ajili ya ukamilishaji wa mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Mnyawa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba
Akikabidhi vifaa hivyo Januari 31,2021 ambavyo vimetolewa na Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika TANECU na mkulima wa korosho Tandahimba Ndg.Karimu Chipola ambapo ametoa mabati 200 na Ofisi ya DC Tandahimba imetoa saruji mifuko 20 ikiwa ni utekelezaji wa ahadi zao kuunga juhudi za wananchi katika ujenzi wa Zahanati hiyo
“Nawapongeza kwa kutekeleza ahadi hizi,lakini namimi pia nitawashirikisha wadau ili kukamilisha ujenzi wa Zahanati ya Mnyawa wananchi waweze kupata huduma karibu na makazi yao,”amesema RC
Naye Ndg.Chipola amesema kuwa mabati hayo ni utekelezaji wa ahadi yake ambayo aliwaahidi wananchi wa kijiji cha Mnyawa kuchangia ujenzi wa Zahanati hiyo ili waweze kupata huduma za afya karibu na makazi yao
Nao wananchi wa kijiji cha Mnyawa kwa nyakati tofauti wamepongeza hatua hiyo ya utekelezaji wa ahadi kwa wakati
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa