Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Kanali Ahmed Abbas Ahmed amesistiza udhibiti Ukusanyaji wa Mapato kwa vyanzo vilivyopo katika Halmashauri na kuendelea kubuni vyanzo vipya ili kuongeza Mapato ambayo yanasaidia katika Utekelezaji wa shughuli za Maendeleo
Rc baada ya kuwasili Halmashauri ya Tandahimba Oktoba 18,2022 alipokelewa na Uongozi wa Wilaya ukiongozwa na Katibu Tawala Ndugu Juvenile Mwambi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba ambapo alipokea taarifa ya Wilaya na kuzungumza na Watumishi
“Nawapongeza kwa kufanya kazi kwa ushirikiano lakini ,muendelee kusimamia na kudhibiti ukusanyaji wa mapato katika vyanzo vilivyopo lakini pia kubuni vyanzo vipya ili kuongeza mapato , wakusanyaji wa mapato muwatambue kwa ufanyaji wa kazi hiyo kwa uadilifu kwa kuwapa vyeti vya shukrani sambamba na motisha zingine,”amesema Rc
Aidha amesema kuwa utatuzi wa migogoro ya ardhi ifanyiwe suluhisho kwa wakati ili kuepuka madhara ambayo yanaweza kujitokeza endapo mgogoro hautatolewa ufumbuzi kwa wakati
Akizungumzia suala la mikopo ya asilimia kumi ambayo inatolewa kwa Wanawake,Vijana na Watu wenye ulemavu amesema kuwa makundi yanayopewa mikopo yasijirudie rudie ili kutoa nafasi kwa makundi mengine yenye uhitaji kupata fedha hizo
Katika kikao hicho Rc amezungumzia hoja za wakaguzi ambazo bado hazijajibiwa zijibiwe ili zifungwe ,usimamizi wa miradi ili kukamilisha kwa wakati na kuangalia fursa za kiuchumi zilizopo kwa wawezeshaji sambamba na ubunifu ili kuzalisha kwa tija
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa