Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe.Kanali Ahmed Abbas Ahmed amepongeza ujenzi wa miundombinu ya mradi wa Shule mpya ya msingi Mambamba Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba
Pongezi hizo amezitoa leo Julai 29,2023 alipotembelea kukagua mradi huo akiwa ameambatana na Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmasahauri zote za Mkoa wa Mtwara
" Nawapongeza mmetekeleza na kusimamia maagizo ya Serikali,Mmenimaliza kabisa sina la kusema zaidi ya kuwapongeza kwa kusimamia mradi wa shule,imejengwa kwa ubora tunamshukuru sana Mhe.Rais ," RC Ahmed
Aidha amesema Serikali inatumia fedha nyingi kutekeleza miradi hiyo ni jukumu la kila mmoja kuilinda na kuitunza
Mradi wa ujenzi wa Shule mpya ya Msingi Mambmba umetekelezwa kwa gharama ya Tsh Mil.331.6 kutoka Serikali Kuu kupitia Mradi wa BOOST ambao utapunguza mlundikano wa wanafunzi shuleni ambapo wananchi wa Mambamba wameishukuru Serikali ya awamu ya sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa