Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe Brig.Jen.Marco Gaguti amesema maeneo ambayo wananchi wamevamia wenyeviti wa vijiji na vitongoji wasitoe namba za anwani za makazi katika maeneo hayo
Ameyasema hayo leo Februari 17,2022 kwenye kikao kazi cha anwani na makazi kwa wenyeviti wa vijiji katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba
“Kwenye maeneo ambayo wananchi wamevamia kama vile kwenye vyanzo vya maji na sehemu za hifadhi na wamejenga wenyeviti wa vijiji msitoe namba za anwani za makazi kwenye maeneo hayo,,”amesema Rc Gaguti
Aidha Rc ameipongeza Wilaya ya Tandahimba kwa kampeni ya ondoa ziro kwa kidato cha nne na kidato cha pili ambapo amesema ana imani kuwa italeta mafanikio makubwa kwa Wilaya na Mkoa Mtwara
“Nawapongeza kwa kuanza kampeni hii ya kuondoa ziro Tandahimba, ni Imani yangu tukilisimamia hili ,tunakwenda kuondoa kabisa ziro ,”amesema Rc Gaguti
Naye Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amesema kuwa katika zoezi la anwani za makazi zipo nafasi za vijana kufanya kazi ya kuingiza taarifa kwenye mfumo ambapo jukumu hilo litatekelezwa katika ngazi ya kitongoji ili kutoa nafasi kwa vijana kushiriki katika maeneo yao
“Katika zoezi hili kuna vijana watahitajika kufanya kazi sisi kama Wilaya tumetoa nafasi zoezi hilo la kuwapata vijana lifanyike katika ngazi za vitongoji ili kuwapa nafasi vijana wetu kufanya kazi hiyo kwa weledi mkubwa na uzalendo wa nchi yao kikubwa awe na sifa ya kuwa na simu janja na awe amemaliza kidato cha nne au kidato cha sita,”amesema Dc Sawala
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ndugu Mussa Gama amesema kuwa anaamini zoezi hilo litakamilika kwa wakati na kwa ufanisi mkubwa baada ya wanyeviti hao kupewa elimu hiyo ya anwani za makazi
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa