Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Brigedia Jenerali Marco Gaguti amesema pembejeo za ruzuku zitumike kama ilivyokusudiwa na serikali ili ziwafikie wakulima zisibaki kwenye maghala
Amesema hayo leo Juni 9,2022 wakati akizungumza na wananchi wa kata ya miuta akiwa katika ziara ya kutembelea na kukagua zoezi la ugawaji wa pembejeo za ruzuku ambapo alitembelea vituo viwili Miuta na Dinduma barabarani
“Wakulima hakikisheni mnaopata pembejeo ni wahusika ambao wapo katika orodha,jukumu hilo ni la wakulima wote wa eneo husika kwa kushirikiana na kamati yenu ya kijiji,anayegawa pembejeo si Rc ,Dc au Kamati ya pembejeo Wilaya sisi tunachofanya ni kusimamia pembejeo hizo ziwafikie wakulima kama ilivyokusudiwa na serikali ,”Amesema Rc
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala(kati) akifafanua jambo kuhusu ugawaji wa zoezi la pembejeo za ruzuku
Aidha Rc ametumia nafasi hiyo kuwapa taarifa ya miradi mikubwa miwili ya barabara na maji ambayo itaanza kutekelezwa na Serikali ya awamu ya sita na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba wakiwa ni miongoni mwa wanufaika wa miradi hiyo
“ Tuna kila sababu ya Kumshukuru Mhe.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miradi hii ambapo mradi wa ujenzi barabara kwa kiwango cha lami lakini pia mradi wa maji kupitia chanzo cha maji Mitema ambapo kiasi cha shilingi Bilioni 100 zitatumika kuboresha miundo mbinu hiyo ili wananchi waweze kupata maji,tunamshukuru sana Rais,”amesema Rc Gaguti
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Robert Mwanawima akisoma taarifa ya zoezi la ugawaji wa Pembejeo za ruzuku kwa RC(hayupo pichani)
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Ndugu Robort Mwanawima akisoma taarifa ya zoezi la ugawaji wa pembejeo amesema kuwa tayari vijiji 74 vimepata pembejeo bado vijiji 84 ambavyo vinaendelea kugawiwa
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa