Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba amekabidhi mabati,saruji ,tanki la maji na mpira vyote vikiwa na thamani zaidi ya shilingi milioni 1.6 kwa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Tandahimba Said Msomoka vifaa ambavyo ni utekelezaji wa ahadi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa
Vifaa hivi ni utekelezaji wa ahadi ya Rc wa Mtwara katika ziara yake ambayo aliifanya Wilayani Tandahimba
Hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika shule ya Sekondari Nandonde ambapo Dc Waryuba amesema kuwa vifaa hivyo ambavyo vimetolewa vitumike kama ilivyokusudiwa na Rc Byakanwa
“Rc ametekeleza ahadi aliyoitoa kwa wananchi wa Tandahimba , kwaiyo jukumu linabaki kwa watendaji kuhakikisha vifaa hivi vinatumika kama ivyokusudiwa na si vinginevyo,”amesema Waryuba
Dc Waryuba (kati)akikabidhi vifaa hivyo kwa Mkurugenzi Mtendaji Said Msomoka (wapili kushoto)
Naye Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Tandahimba Said Msomoka amesema vifaa hivyo wahusika watavitumia kama ilivyokusudiwa ili kuleta maendeleo kwa shule na kwa Wilaya ya Tandahimba
“Tunamshukuru Rc kwa utekelezaji wa ahadi yake,nami naahidi vifaa vitatumika kama ilivyokusudiwa kwa walengwa kama saruji na mabati zitatumika katika kumalizia mradi wa choo Sekondari ya Nandonde na Mihambwe ,vile vile tanki la maji na mpira vitatumika ipasavyo maeneo kusudiwa,”amesma Msomoka
Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Chikongo Abdallah Bakar(kushoto)i wakati akipokea tanki la maji
Aidha Afisa Elimu Msingi (W)Hadija Mwinuka amemshukuru Rc na kueleza kuwa Tandahimba ni Halmashauri inayofanya vizuri kati ya halmashauri za Mkoa wa Mtwara kwenye zoezi la kampeni ya ‘Shule ni choo’
Afisa Elimu Msingi (W) Hadija Mwinuka akitoa shukrani kwa Rc kwa kutekeleza ahadi hiyo ya vifaa
“Tunashukuru Rc kwa kutekeleza ahadi yake kwenye kampeni ya Shule ni choo na sisi Tandahimba ni miongoni mwa Halmashauri ambayo utekelezaji wake umekuwa na hamasa kubwa,”amesema Mwinuka
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa