Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa ameipongeza Halmashauri ya Tandahimba kwakupata hati safi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za serikali (CAG) kwa mwaka 2018/2019
Ameyasema hayo leo kwenye kikao maalum cha Baraza la Madiwani la kujadili taarifa ya mdhibiti na mkaguzi kuu wa hesabu za serikali(CAG) ambalo limefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Tandahimba
RC Gelasius Byakanwa(Kulia) akiwa na Dc Sebastian Waryuba (kushoto) kwenye kikao maalum cha baraza la madiwani
“Naipongeza Halmashauri ya Tandahimba kwa kupata Hati safi kwa mara nyingine tena,kiongozi wa Mkoa unapata usingizi ikiwa Halmashauri zako zinapata hati safi, nazitaka Halmashauri zote kupata hati safi ifike mahali hati chafu abaki naye yeye CAG ili sisi ijulikane kuwa ni waelewa na tunafuata utaratibu,”amesema Byakanwa
Kamati ya ulinzi na Usalama,Wakuu wa Idara na Vitengo ambao walihudhuria baraza hilo
Aidha amesema wataalamu wahakikishe wanakusanya mapato kwakuwa ndiyo uti wa mgongo wa Halmashauri kwa mwaka 2018/2019 ilikadiriwa kukusanywa Bilioni 5 lakini makusanyo yaliyopatikana ni shilingi Bilioni 1 hivyo jitihada zifanywe ili kuhakikisha mapato yanaongeza
“Hatuwezi kuendelea kuwachekea watu wanaokaa na fedha za mapato mifukoni badala ya kuja kwenye Halmashauri ili fedha hizo zirudi kwenye miradi ya maendeleo kwa wananchi,miradi mikubwa mnayoiona ni usimamizi mzuri wa ukusanyaji wa mapato ,”amesema Byakanwa
Madiwani wa Halmashauri ya Tandahimba wakiwa kwenye kikao maalum cha kujadili taarifa ya CAG
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Namkulya Namkulya amesema kuwa ndani ya miaka minne mfululuzo Halmashauri ya Tandahimba imepata hati safi hiyo ni kudhihirisha taratibu na kanuni za fedha zinafuatwa
Mwenyekiti wa Baraza la Halmashauri ya Tandahimba Namkulya Namkulya (kulia) akielezea jambo (kushoto) Rc Byakanwa
“Hii ni mara ya nne kupata hati safi mfululizo kwa Halamsahuri yetu kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuanzia tumeingia madarakani sisi madiwani,tunafarijika kwa jambo hili,”amesema Namkulya
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa