Kaimu Mkuu wa Mkoa Sebastian Waryuba akimkabidhi Afisa Elimu Msingi Hadija Mwinuka Hati ya Makabidhiano ya shule ya Luagala 'B'
Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Zaidi ya Shilingi Milioni 154 zimetumika katika kujenga vyumba vitatu vya madarasa na ukarabati wa shule ya msingi Luagala B sambamba na kisima cha maji chenye ujazo wa Lita 150,000 kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya wananfunzi
Akizindua madarasa hayo Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Sebastian Waryuba alieleza kuwa madarasa yamekamilika pamoja na madawati
Katika vyumba vitatu hivyo wanafunzi watasoma katika hali ya amani jukumu limebaki kwa wananfunzi kusoma kwa bidii na kuitunza miundo mbinu hiyo
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Sebastian Waryuba akiwa na wafadhili wa mradi taasisi ya ECLAT na Upendo
Alisema Mradi huo ambao umetekelezwa na Taasisi ya Eclat na Upendo chini ya Meneja wa Mradi ambaye ni mzawa wa kijiji cha Luagala B
umekabidhiwa kwa serikali na jukumu linabaki kwa wanakijiji kuitunza miundombinu ya shule
“Mradi huu ni wa fedha nyingi,tunawaomba wananchi wa kijiji hiki muutunze ili vizazi vijavyo na vijavyo vitumie,tunawashukuru taasisi hizi mbili Eclat kutoka Simanjiro Tanzania na Upendo kutoka Ujerumani ambao wametekeleza mradi huu,lakini tunamshukuru mzawa Msham Bashir ambaye amewaleta huku katika kijiji alichotoka kwa ajili ya kuboresha miundo mbinu ya Elimu,”alisema Waryuba
Shule ya Msingi Luagala 'B' ikiwa na muonekano mpya baada ya mradi kukamilika
Naye Mwenyekiti wa Taasisi ya ECLAT Toima Kiroya alieleza kuwa katika mradi huo ambao wameutekeleza ni ukarabati wa majengo 8,ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa,kisima chenye ujazo wa lita 150,000,madawati 65,matundu ya choo 16,Meza za walimu 16 na viti 16
Mbali na hilo naye Dk Fred Heimbach wa Upendo Society kutoka Ujerumani alieleza kuwa madhumuni ya ushirika huo ni kuboresha sekta ya elimu katika upande wa Miundo Mbinu hivyo inatakiwa itunzwe ili iendelee kuwa msaada kwa vizazi vijavyo
Dk Fred Heimbach wa Upendo Society akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Eclat Toima Kiroya
Hata hivyo Meneja wa Mradi huo Msham Bashir alieleza kuwa anaishukuru Serikali kwa kushirikiana nao kuanzia ngazi ya Shule,kijiji hadi
Wilaya na wananchi wa Luagala
Meneja wa Mradi (Mzawa) Msham Bashir akiishukuru serikali na wananchi kwa ushirikiano
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa