Na Kitengo Cha Habari na Mawasiliano
Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara ndugu Abdallah Malela amewataka wasimamizi wa miradi ya vyumba vya madarasa katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba kuhakikisha mafundi wanaongeza kasi katika utekelezaji wa miradi hiyo ili ikamilike kwa wakati
Ras(aliyevaa kofia)akikagua ujenzi wa vyumba sita vya madarasa sekondari ya Dinduma
Ameyasema hayo Novemba 19,2021 kwenye ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa akiwa pamoja na timu ya ufuatiliaji Wilaya ikiongozwa na Katibu Tawala Wilaya ndugu Juvenile Mwambi
Ras akitoa maelekezo kwa kamati katika shule ya sekondari ya Naputa
“Wasimamizi ambao mpo katika maeneo ya miradi hakikisheni mafundi wanaanza kazi mapema ili miradi hii ikamilike kwa wakati,lakini mkiwaacha mafundi waamue wenyewe watakwamisha kukamilika kwa wakati,sisi tuna haraka na miradi hii,”amesema Ras
Naye Katibu Tawala Wilaya ya Tandahimba ndugu Juvenile Mwambi amesema kuwa timu za ufuatiliaji ngazi ya Wilaya zinapita katika miradi hiyo kuhakikisha inakwenda kwa kasi ili iweze kukamilika kwa wakati uliopangwa
Aidha nao mafundi viongozi katika miradi ambayo amepita kukagua Katibu Tawala Mkoa wamemuhakikishia kuwa wataimaliza miradi hiyo kwa wakati ili malengo ya Serikali yaweze kutimia
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa