Na Kitengo cha Mawasiliano
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaendelea kutoa Pembejeo za ruzuku ili kuwawezesha wakulima wa zao la Korosho kuzalisha kwa wingi na kukuza Uchumi wa mkulima na Taifa kwa ujumla.
Dkt.Samia ameyasema hayo leo Septemba 16,2023 kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Uwanja wa mpira wa Majaliwa akiwasisitiza wagawaji wa pembejeo hizo kusimamia ugawaji wenye tija kwa wananchi.
"Lengo la pembejeo za ruzuku ni kuongeza uzalishaji wa zao la korosho kwa wingi ili mkulima aweze kukuza uchumi wake na Taifa lakini kama uzalishaji unapungua ugawaji wa pembejeo za ruzuku hautakuwa na tija kwa mkulima," amesema Mhe.Rais
Kwa upande wa miradi ya maendeleo Mhe.Rais amewasistiza Madiwani wa Halmashauri na viongozi kusimamia miradi hiyo ambayo Serikali inatoa fedha nyingi kuitekeleza.
Aidha katika sekta ya ya Elimu amesema kuwa Serikali imeboresha miundombinu ya Elimu na kutoa elimu bure kwa wanafunzi kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha sita hivyo ni wajibu wa kuwasimamia watoto kwenda shule
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan yuko katika ziara Mkoani Mtwara akitembelea miradi na kuzungumza na wananchi
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa