Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Watendaji kata Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba wametakiwa kuongeza kasi katika ukusanyaji wa mapato ya ndani baada ya kukabidhiwa pikipiki 32 zenye thamani ya zaidi ya shilingi Mil.83 fedha ambazo zimetokana na mapato ya ndani
Mwenyekiti Mhe.Baisa Baisa akimkabidhi pikipiki katibu wa watendaji ndugu Sudi Sudi
Akikabidhi pikipiki hizo 32 kwa watendaji kata zote Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Mhe.Baisa Baisa ameeleza kuwa fedha zilizotumika kununulia pikipiki hizo zimetokana na mapato ya ndani lakini ziliwekwa kwenye bajeti ya kununua gari ya Mkurugenzi
Amesema kuwa Mkurugenzi baada ya kuona changamoto iliyopo katika ukusanyaji wa mapato akaridhia fedha hiyo isinunuliwe gari badala yake itumike kuwanunulia vyombo vya usafiri watendaji kata ili ziwasaidie katika ukusanyaji wa mapato
“Nampongeza Mkurugenzi kwa kuridhia na madiwani naamini pikipiki hizi zinakwenda kuleta matokeo mazuri katika ukusanyaji wa mapato ndani ya Wilaya yetu,hatutarajii kusikia tena changamoto ya usafiri kutoka eneo moja kwenda jingine kukusanya mapato,mkazitunze kwakuwa ni mali ya uma,”amesema Mwenyekiti
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ndugu Mussa Gama amesema kuwa pikpiki hizo zitawarahisishia watendaji kata kutekeleza majukumu yao ipasavyo hussan ya ukusanyaji mapato ambayo ni lengo kuu
Mkurugenzi Mtendaji ndugu Mussa Gama akiwasha moja ya pikpiki hizo kwa ajili ya majaribio
“Fedha hizi zilitakiwa zinunue gari,lakini nikaona kuwa tuboreshe ukusanyaji wa mapato,watendaji ndiyo wanahusika wa zoezi hilo katika maeneo yao,nikaridhia na nikawashawishi madiwani pia tubadili matumizi haya ili tuongeze mapato ya Halmashauri yetu,lakini pia pikipiki hizi zitawasaidia kufika kwa wakati katika vikao mbalimbali ambavyo wanahitajika Wilayani,kwasababu wengi walikuwa wanachelewa kutokana na changamoto ya usafiri,”amesema Mkurugenzi
Aidha nao watendaji kata ambao leo wamekabidhiwa pikipiki hizo wameushukuru Uongozi wa Halmashauri lakini pia wamesema usafiri kutoka eneo moja kwenda lingine ilikuwa ni changamoto katika kutekeleza majukumu yao
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa