Baraza la madiwani na wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba wakiwa katika maeneo mbalimbali Visiwani Zanzibar ambapo pamoja na kujifunza Ukusanyaji wa Mapato, uendeshaji na usimamizi wa masoko katika eneo la Forodhani, wametembelea maeneo mbalimbali ya kihistoria ikiwemo Ngome kongwe, Maeneo ya Makaburi .
Wakiwa visiwani humo Madiwani na wataalamu wametembelea Ofisi za CCM Zanzibar na kujifunza historia mbalimbali za Viongozi akiwemo Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume sambamba na kutembelea Kaburi lake, Kanisa la Mkunazini ambalo lilikuwa likitumika kama soko kuu la Watumwa Afrika Mashariki.
Aidha, ziara hiyo ya siku tatu inaendelea Leo Januari 15 na itahitimishwa Januari 16 2025 ambapo inatarajiwa kuleta tija kwa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba hasa katika kuongeza Mapato ya Halmaykwa kuboresha vitega Uchumi ikiwemo soko la forodhani ambalo pia liko Tandahimba.
#tandahimba tumejipanga, kazi zinaendelea
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa