Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Operesheni ya anwani ya makazi inaendelea katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ambapo mitaa mbalimbali imewekwa vibao na tayari nyumba zimewekwa namba
Kibao kikionyesha mtaa wa Brig.Jen Gaguti uliopo kitongoji cha sokoni kata ya Tandahimba
Wananchi wa Tandandahimba kwa nyakati tofauti wameipongeza serikali kwa hatua hiyo na kuongeza kuwa itarahisisha huduma nyingi za maendeleo katika mitaa,vitongoji na Wilaya kwa ujumla
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe.Brig.Jen.Marco Gaguti alitembelea baadhi ya mitaa ukiwemo mtaa wa gaguti ambapo wakazi wa eneo hilo wamemuenzi kwa kuupa mtaa huo jina lake kwa kutambua mchango wake katika shughuli za maendeleo
“Nawapongeza mmejitahidi kufanya operesheni hii kwa wakati na mmekamilisha kama mtaa hongereni sana,nashukuru kwa kunipa heshima hii mimi nimekuwa mmoja wa wakazi wa mtaa huu, mnishirikishe katika maendeleo ya mtaa wetu ,nachangia shilingi milioni 2 kwa ajili ya maendeleo ya elimu katika shule yetu iliyopo ndani ya kata yetu ya Tandahimba,”amesema Rc
Aidha naye Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala ametembelea na kukagua operesheni hiyo katika maeneo mbalimbali na kuridhishwa na utendaji kazi wa viongozi katika kutekeleza jukumu hilo
Hata hivyo Kamati ya uratibu wa anwani za makazi Wilaya inaendelea kutembelea na kukagua operesheni hiyo katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ili kutatua changamoto zinazojitokeza
Mjumbe wa kamati ya uratibu wa anwani za makazi Wilaya ndugu Joseph Mongi akimuelekeza jambo mtendaji wa kijiji cha mkula
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa