Na Kitengo cha Mawasiliano
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba zimetoa majiko 100 ya gesi na kukabidhi kwa baba lishe na mama lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ili kuboresha na kulinda mazingira kwenye maeneo yao ya kazi.
Majiko hayo yamekabidhiwa leo Desemba 10,2024 na Mhe Kanali Michael Mntenjele kwenye maadhimisho ya kilele cha kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili ambayo yameadhimishwa shule ya msingi Dinduma Kata ya Dinduma Halmashauti ya Wilaya ya Tandahimba.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti mara baada ya kukabidhiwa majiko hayo baba lishe na mama lishe hao wameishukuru Serikali kwa majiko hayo ambayo wamesema yatakwenda kuongeza ufanisi wa shughuli zao za kila siku.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa