Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amepokea mabati 369,madawaati 390 na stuli za maabara 100 zote zikiwa na thamani ya Tsh Milioni 63.9 kutoka Benki ya NMB tawi la Tandahimba ikiwa ni mchango wao kwa sekta ya elimu kuunga juhudi za Serikali katika sekta hiyo.
Akizungumza Novemba 7,2023 kwenye Hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa hivyo yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri na kuhudhuriwa na Wakuu wa Idara na watumishi Dc Sawala ameipongeza benki ya NMB kwa vifaa hivyo ambapo amesema vitasaidia katika ujifunzaji na ufundishaji katika shule hizo.
" Nawapongeza sana Benki ya Nmb kwa mchango huu wa madawati,mabati na stuli za maabara ambazo zinakwenda kupunguza uhaba kwenye shule zetu,wito kwa taasisi nyingine kuiga mfano wa NMB wa kurudisha kwa jamii,ili kuendelea kuunga juhudi za Serikali katika Sekta ya Elimu" amesema Dc Sawala.
Kwa upande wake Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kusini Ndg.Faraja Ng'ingo akikabidhi vifaa hivyo amesema kuwa benki hiyo imekuwa na utaratibu wa kurudisha faida ya asilimia 1 wanayoipata kwa jamii ambapo wanachangia katika sekta ya Elimu na Afya kama sehemu ya uwajibikaji kwa jamii inayowazunguka.
" Tunatambua juhudi za Serikali ya awamu ya sita ya kusimamia upatikanaji wa Elimu bora kwa nguvu zote,hatuna budi kuipongeza Serikali kwa hilo na sisi kama wadau tunao wajibu wa kuunga mkono juhudi hizi za Maendeleo kwani jamii imeifanya Benki ya NMB kuwa hapa tulipo," amesema Meneja wa Kanda
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa