Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandhimba Mhe Kanali Patrick Sawala amepokea mabati 400 yenye thamani ya Tsh.17,200,000,000(Shilingi Milioni kumi na saba na laki mbili) kutoka Benki ya NMB tawi la Tandahimba
Akipokea vifaa hivyo vya uendelezaji wa kituo cha Mnyawa na Zahanati ya Nachunyu Oktoba 10,2022 Dc Sawala amewapongeza Benki ya NMB kwa jnsi ambavyo inaunga mkono juhudi za Serikali katika shughuli mbalimbali za Maendeleo
‘Tunawapongeza benki ya NMB kwa kutoa mabati 400 ambayo kila kituo kimepata mabati 200,Nmb wamekuwa wadau wetu wa maendeleo katika Wilaya yetu ambapo inatoa vifaa katika sekta ya Elimu na Afya,tunawashukuru ,”amesema Dc Sawala
Aidha ametoa woito kuhakikisha mabati ambayo yamekabidhiwa yanafanya kazi iliyokusudiwa na si vinginevyo ambapo amewasistiza wananchi kuendelea kushiriki katika shughuli za ujenzi ili vituo hivyo vikamilike na kuanza kutoa huduma
Naye Meneja wa Kanda ya Kusini wa Benki ya NMB Bi.Janeth Shango amesema kuwa ni utaratibu wa benki hiyo kutoa sehemu ya faida inayopata kurudisha kwa jamii ili kuunga juhudi za Serikali katika kuwaletea wananchi Maendeleo
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa