Na Kitengo cha Mawasiliano.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Mhe.Baisa Baisa ameishukuru Benki ya NMB Tawi la Tandahimba kwa kutoa vifaa vyenye thamani ya Tsh.Milioni 63.9 kusaidia Sekta ya Elimu Tandahimba.
Akizungumza kwenye Hafla ya makabidhiano Novemba 7,2023 Mhe.Baisa amesema benki ya NMB imekuwa mstari wa mbele kuchangia maendeleo katika sekta ya Elimu na Afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba .
" Tunaishukuru Benki ya NMB kwa ushirikiano wao na misaada wanayoitoa kwa Halmashauri yetu kwa ajili Maendeleo ya Sekta ya Elimu ambayo ni kipaumbele kwa Maendeleo ya Taifa letu," amesema Mhe.Baisa
Shule zilizopata msaada huo ni Shule ya Msingi Chikongo Madawati 50,,Shule ya Msingi Chikongola madawati 50,Shule ya Msingi Michenjele madawati 100, Shule Msingi Nachunyu madawati 50,Shule ya Msingi Mtegu madawati 50,Shule ya Msingi Namdwani madawati 50,Shule ya Msingi Mitondi madawati 50.
Aidha Benki ya NMB,imetoa msaada wa Stuli za Maabara 100 kwa Shule ya Sekondari Chaume na mabati 396 ambayo yametolewa kwa shule za msingi nne ambazo ni Shule Msingi Malamba,Shule Msingi Kunandundu,Shule Msingi Ukombozi na Shule ya Msingi Chilinda.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa