Na .Kitengo cha Mawasiliano
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Mhe.Baisa Baisa amegawa vifaa vya shule vyenye thamani ya shilingi Milioni moja na laki tano (1,500,000) kwa wanafunzi wa darasa la kwanza kwa shule tano za msingi zilizopo Kata ya Kitama
Akikabidhi vifaa hivyo Januari 17,2023 katika shule hizo Mhe.Baisa amesema kuwa vifaa hivyo vitawasaidia wanafunzi hao wawapo darasani
“Nimefanikiwa kugawa vifaa kwa wanafunzi wa darasa la kwanza katika shule tano ambazo zipo katika kata ya Kitama ni imani yangu vifaahivi vitakuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi wetu kusoma na kuandika wawapo darasani,”amesema Mwenyekiti
Aidha amevitaja vifaa hivyo kuwa ni madaftari,penseli,ufutio na vichongeo ambapo shule ya Mitondi ,Mitondi A,Mwenge,Namunda na Kitama zimepata vifaa hivyo
Nao walimu wa shule hizo kwa nyakati tofauti wamempongeza Mwenyekiti kwa hatua hiyo
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa