Na Kitengo cha Mawasiliano.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Tandahimba Mhe.Ismaili Mkadimba amewataka wanafunzi kuzingatia masomo ili wafikie malengo waliyojiwekea.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Namikupa Oktoba 4,2023 mara baada ya Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Tandahimba ikiongozwa na Mwenyekiti Mhe.Ismaili Mkadimba kukagua mradi wa ujenzi wa bweni la Wasichana Shule ya Sekondari Namikupa
"Zingatieni masomo ili muweze kufikia malengo yenu,Serikali ya Awamu ya Sita imeboresha Miundombinu ya Elimu ili msome kwenye mazingira bora, jukumu lenu wanafunzi ni kuongeza bidii kwenye masomo,msijiingize kwenye mambo mengine ambayo yatawakatishia masomo yenu," amesema Mhe.Mkadimba.
Aidha,amepongeza miradi iliyokamilika na kusistiza ianze kutoa huduma kwa wananchi lakini pia ameagiza miradi ambayo bado isimamiwe iweze kukamilika kwa wakati ili wananchi waweze kupata huduma.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amesema maelekezo yaliyotolewa na Kamati ya Siasa ya CCM atayasimamia ili yatekelezwe kwa wakati na wananchi wa Tandahimba waendelee kupata Maendeleo.
Wajumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Tandahimba wamehitimisha ziara yao ya siku mbili Oktoba 4,2023 ambapo wametembelea na kukagua Jumla ya miradi yenye thamani ya zaidi ya Tsh.Bilioni 7.5
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa