Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ametoa agizo la ununuzi wa mashine 3 za kukamulia mafuta ya alizeti kwa muda muafaka ili kuwawezesha wakulima kupata huduma hiyo ndani ya Wilaya
Amesema hayo katika baraza la madiwani la siku mbili lililofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri baada ya ya baadhi ya madiwani kuhoji hatma ya wakulima ambao wamelima zao hilo kwa wingi
Wakuu wa Idara na vitengo wakifuatilia kikao cha baraza la madiwani
“Wakulima wetu tuliwahimiza walime mazao mbadala kama alizeti na ufuta,tunashukuru matokeo ya zao hilo yamekuwa makubwa kwa wakulima wetu,naagiza Halmashauri kuhakikisha mashine hizo za kukamua mafuta ya alizeti yanafungwa haraka ili wakulima wakivuna waweze kupata huduma hiyo ndani ya Wilaya ya Tandaahimba,’amesema Mwenyekiti
Baraza la madiwani wakiwa katika kikao cha robo ya tatu
Aidha katika baraza hilo madiwani wamewasilisha na kujadili taarifa za utekelezaji wa maendeleo ya kata zao sambamba na uwasilishaji wa taarifa mbalimbali za kamati za kudumu katika kipindi cha robo ya tatu
Katika kikao hicho baraza la madiwani lilipongeza taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ndugu Mussa Gama kwa kuwezesha utekelezaji wa ufungaji wa taa za barabarani zenye thamani ya shilingi Milioni 140
“Nachukua nafasi hii kumpongeza Mkurugenzi kwa kufanikisha ufungaji wa taa za barabarani na kuifanya Tandahimba kuwa na muonekano tofauti na wakuvutia hasa usiku,”amesema Mhe,Hamza Balakali Diwani wa kata ya Kwanyama
Naye Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala ametoa wito kwa baraza la madiwani kuhamasisha wananchi katika kata zao kushiriki katikaa zoezi la sensa ya watu na makazi Agosti 23,2022
Dc Sawala akisistiza suala la sensa katika kikao cha baraza la madiwani
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa