Na Kitengo cha Mawasiliano
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2023 Ndugu.Abdalla Shaib Kaim ameridhia miradi ya maendeleo ambapo amezindua miradi miwili na kuweka jiwe la msingi miradi mitatu
Miradi ambayo imezinduliwa Aprili 5,2023 ni ujenzi wa nyumba ya watumishi wa afya(3 kwa 1) hospitali ya wilaya ya Tandahimba ambapo gharama ya mradi huo ni shilingi Milioni tisini (90,000,000)fedha kutoka Seikali kuu ambao utarahisisha watumishi kutoa huduma kwa wakati
Mradi mwingine ambao umezinduliwa na Mwenge wa Uhuru ni ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa shule ya Sekondari ya Tandahimba ambao thamani yake ni shilingi milioni themanini(80,000,000) fedha kutoka Serikali kuu
Aidha Mwenge wa Uhuru umeweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kubangua korosho cha Organic growth ambapo gharama ya mradi shilingi bilioni tatu na milioni miatano (3,500,000,000),umeweka jiwe la msingi Mradi wa ujenzi wa ofisi ya Uhamiaji wilaya ya Tandahimba wenye gharama ya shilingi milioni milioni mia mbili ishirini na tisa laki saba tisini na mbili na mia tatu kumi na tano (229,792,315)
Pia Mwenge wa Uhuru umeweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa barabara ya lami Km 1.715 ambao gharama yake ni shilingi Milioni mia tisa hamsini (950,000,000) na wameona vikundi vilivyopata mkopo wa Halmashauri ambapo kiasi cha shilingi milioni mia moja hamsini(150,000,000) zimetolewa kwa vikundi ili kuwawezesha kiuchumi
Kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 “Tunza Mazingira Okoa Vyanzo vya Maji kwa Ustawi wa Viumbe hai na Uchumi wa Taifa”
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa