Mwenge wa Uhuru umeridhia kuweka jiwe la Msingi Barabara ya Kavende-Msikitini na Taifa Teule -Bus Stand yenye urefu wa Kilomita 1.13 kiwango cha Lami.
Akizungumza wakati wa kuweka jiwe la Msingi Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu Godfrey Mzava amesema Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuboresha miundombinu ya barabara na ndio maana anatoa fedha Kwa ajili ya utekelezaji wa miundombinu hiyo kwa Wananchi akisisitiza utunzaji wa Barabara hizo ili ziweze kudumu kwa Muda mrefu.
Mradi huo umegharimu kiasi Cha Tsh.Milioni 949.4 na Ujenzi umefikia 90% na unatarajia kukamilika ifikapo Juni 14, 2024.
Kaulimbiu:"Tunza Mazingira na Shiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu "
#kaziiendelee
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa