Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu Wilaya yaTandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amemkabidhi baiskeli Mwalimu Ndg Bakari Kuwandu ambaye ni mlemavu anayefundisha shule ya Msingi Mjimpya iliyopokaa ya Tandahimba
Akimkabidhi baiskeli hiyo Septemba 22,2022 katika shule ya msingi Mjimpya, Dc Sawala amesema kuwa alipokea maombi yake ya uhitaji wa baiskeli ofisinikwake Septemba 19,2022
“Nilipokea maombi yake wiki hii ambapo alisema kuwa baiskeli ambayo alikuwa akiitumia ni mbovu,nikalichukulia jambo hili kwa uzito mkubwa ukizingatia baiskeli inamsaidia kuingia darasani kuwafundisha wanafunzi wetu ,nikawasaliana na wadau nimeipata nimekuja kumkabidhi ili iweze kumsaidia,”amesema Dc Sawala
Naye Mwalimu Bakari Kuwandu amemshukuru Dc kwa kumkabidhi baiskeli hiyo na ameipongeza Serikali kwa kuwajali watu wenye ulemavu “Nashukuru sana Mhe.Dc Sawala ni juzi tu nimepeleka maombi yangu ofisini kwake lakini leo amekuja kunikabidhi baiskeli,asante sana,”amesema Mwalimu Kuwandu
Aidha akiwa shuleni hapo Dc Sawala amewasistiza wanafunzi kuweka juhudi katika masomo yao ili waweze kufikia malengo yao na amewapongeza walimu washule hiyo kwa kazi kubwa wanayofanya na kuhakikisha wanafunzi wanafanya vizuri
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa