Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wlaya ya Tandahimba ndg Said Msomoka amewataka wajumbe wa Kamati ya Mpango wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) Wilaya ya Tandahimba kutekeleza kwa vitendo mpango huo kwenye maeneo yote ndani ya Wilaya
Wajumbe wa kamati ya MTAKUWWA Tandahimba wakipatiwa mafunzo
Ameyasema hayo kwenye mafunzo ya siku tano ya kamati ya MTAKUWWA wilaya ya Tandahimba ambayo yamefanyika katika ukumbi wa mdogo wa mikutano wa Halmashauri ya Tandahimba.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya yaTandahimba Ndg.Said Msomoka ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati hiyo akitoa neno kwa wajumbe
“Kamati hii natumaini mtakwenda kuleta mabadiliko katika jamii kwakuwa wajumbe ni wataalam na wengine mmetoka katika asasi mbalimbali hivyo mafunzo yatalete mabadiliko ndani ya jamii zetu,”amesema ndg.Msomoka
Aidha naye mwezeshaji wa Kitaifa wa mafunzo hayo Dereck Rugina amesema kuwa mada mbalimbali ambazo wajumbe wamefundishwa ikiwemo ulinzi na usalama kwa mtoto zitakwenda kuleta matokeo chanya kwa wajumbe kwa kufikisha elimu hiyo ngazi ya kata,mitaa na vijiji
Mwezeshaji Dereck Rugina akitoa mafunzo kwa wajumbe wa kamati ya MTAKUWWA
Amesistiza kuwa jukumu la kumlinda mtoto ni la jamii nzima hivyo wananchi wakishirikiana kwa pamoja wataendelea kumlinda mtoto na vitendo vya ukatili ambavyo wanafanyiwa katika maeneo mbalimbali
Mwenyekiti wa mafunzo akitoa neno kwa niaba ya washiriki wote wa mafunzo hayo
Akizungumza kwa niaba ya washiriki wote mwenyekiti wa mafunzo hayo amesema kuwa mafunzo yataleta mabadiliko makubwa katika kupinga ukatili dhidi ya watoto kwenye maeneo mbalimbali ya Tandahimba.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa