Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Halmashauri ya Tandahimbas Ismaely Mbilinyi amewataka wasimamizi wanaokwenda kusimamia malipo kwa kaya maskini kuzingatia na kufuata taratibu za fedha katika malipo hayo
Wasimamizi wa kusimamia malipo kwa kaya maskini wakika katika mafunzo
Ameyasema hayo leo tarehe 15/2/2021kwenye semina elekezi wakati akitoa mafunzo kwa wasimamizi hao kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri
“Katika malipo ambayo mnakwenda kufanya mnatakiwa kumlipa mlengwa si mtu mwingine mlengwa mwnyewe ndiye muhusika mkuu katika zoezi hili hii itatusaidia kufuata taratibu za kifedha katika malipo haya,”amesema Mratibu
Mratibu wa TASAF Tandahimba Ismaely Mbilinyi akitoa mafunzo kwa wasimamizi wa kusimamia malipo kwa kaya maskini
Aidha amesema kuwa zoezi hilo la malipo litaanza tarehe 16/2/2021 na litamalizika tarehe 19/2/2021 ambapo awali shughuli hizo zilikuwa zinafanywa na kamati za jamii lakini kwa sasa mfumo huo umebadilika na unafanywa na watumishi wa Halmashauri
Wasimamizi wa kusimamia malipo kwa kaya maskini wakimsikiliza mwezeshaji wa semina hiyo
Wasimamizi wa malipo hayo kwa nyakati tofauti wamesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia katika maeneo yao na hivyo kutekeleza majukumu kwa kufuata taratibu na kanuni zinazohitajika katika zoezi hilo
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa