Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Kaya 30 katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba zimepata kuku wa mayai kwa msaada wa mradi wa kupunguza umaskini na kuongeza kipato kupitia ufugaji ambapo kuku 600 wametolewa kwa kaya hizo
Wananchi wakipokea kuku aina ya saso na kuroila
Akizungumza na wananchi hao kabla ya kuwakabidhi kuku hao Daktari mtafiti wa mifugoEmmanuel Mahenga amesema kuwa mradi unawezeshwa na serikali ili jamii iweze kuongeza kipato kupitia ufugaji
Mkazi Nanhyanga akifurahia mradi wa kuku
“Tunawapa kuku wa aina mbili saso na kuroila muwafuge ili kupunguza umaskini na kuongeza kipato cha familia na zao linalopatikana katika ufugaji kama vile mayai yatasaidia kupata fedha na kutumika kula ili kuwa na afya njema,”amesema Dk Mahenga
Naye afisa Mifugo Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Robert Mwanawima amesema kuwa wataendelea kuwafatilia kuku hao kwa kuwapa matibabu na ushauri pale ambapo itajitokeza kuna tatizo lolote ili waweze kuleta tija kwa jamii hiyo
Afisa Mifugo Robert Mwanawima akipongezwa na mwananchi baada ya kutoa maelekezo ya ufugaji
Mkoa wa Mtwara mradi huo unatekelezwa kwa Halmashauri tatu ikiwemo Tandahimba ambapo vijiji vya Mihule,Nanhyanga A na Nanhyanga C ni miongoni mwa vijiji ambavyo vimefikiwa
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa