Mratibu wa TASAF Judith Mzava pamoja na Afisa Ufuatiliaji TASAF Wilaya ya Tandahimba Rahel Kyomo wamemtembelea Mlengwa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ambae amekuwa akinufaika na fedha zinazotolewa na Serikali kupitia Mfuko huo.
Akizungumza nyumbani kwake Leo Bi.Amina Chihonde Mkazi wa Kijiji Cha Namdowola Kata ya Nanyanga Wilayani Tandahimba amesema kabla ya kupata fedha za TASAF alikuwa na maisha duni.
" Mimi maisha yangu yalikuwa magumu sana, sikuwa na kitu chochote cha kunipatia kipato, lakini baada ya kupata fedha za TASAF sasa naweza kuwasomesha wajukuu zangu, na kuitunza familia yangu vizuri, pia kupitia Fedha za TASAF nimeweka akiba na nimeweza kununua Ng'ombe watatu wa Maziwa ambapo nauza maziwa na kuongeza kipato Cha Familia yangu" Bi Amina.
Kwa Upande wake Afisa Ufuatiliaji TASAF Wilaya ya Tandahimba Rachel Kyomo amesema Serikali inaendelea kutoa fedha nyingi kwa ajili ya Kunusuru kaya maskini akionya baadhi ya Walengwa kuzitumia vyema ili ziwasaidie.
Aidha, Mkuu wa Kitengo Cha TASAF Wilaya ya Tandahimba Judith Mzava amesema wanaendelea kufatilia wanufaika kwa kuelimishwa kujiunga na njia za malipo kwa njia ya simu, kwa mitandao ya Vodacom, Airtel, Halopesa, Tigo pesa, na taasisi za fedha za Benk za NMB na CRDB na kutoa Elimu ya namna ya kuzitumia fedha hizo ili ziwasaidie kujikwamua kiuchumi na kuongeza kipato.
Katika Mwaka wa Fedha 2023/2024 Serikali imetoa Tshs. Bilioni 1.16 kwa kaya maskini 5,859 katika vijiji 157 vya Wilaya ya Tandahimba.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa