Na Kitengo cha Mawasiliano
TANECU imefanya Mnada wa Tatu wa zao la Korosho kwa Msimu wa kilimo Cha Korosho 2023/2024 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ambapo Korosho imeuzwa kwa Bei ya juu ya Tsh.2150 na Bei ya Chini Tsh.2,050 Kwa kilo moja.
Mwenyekiti wa TANECU Karim Chipola amewapongeza Wakulima kwa kuziandaa Korosho kwa Ubora kabla ya kuzipeleka ghalani hali iliyopelekea kiwango cha Wanunuzi kuongezeka ikilinganishwa na Minada miwili iliyopita.
"Leo mnaona tumeuza Tani zote 12,879 hii ni kwa sababu ya usimamizi bora wa korosho zenye ubora kuanzia kwa Mkulima, AMCOS, Viongozi wa Serikali na Viongozi wa Ushirika ...niwaombe tuendelee kushirikiana kutimiza wajibu kila mtu kwa nafasi yake " Chipola
Jumla ya Tani 12,879 zimekusanywa na kuuzwa katika Ghala la Tandahimba na Newala.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa