Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe.Kanali Ahmed Abbas Ahmed amewataka maafisa ugani waliokabidhiwa pikipiki kuzitumia kama ilivyokusudiwa ili kutoa elimu na ushauri wa kitaalamu kwa wakulima waweze kuongeza uzalishaji sambamba na kuzingatia sheria ,taratibu na kanuni za matumizi ya vifaa vya Serikali
Amezungumza hayo Machi 10,2023 wakati akikabidhi pikpiki 34 kwa maafisa ugani katika kijiji cha Nanhyanga Kata ya Nanhyanga Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ambapo Pikipiki hizo zimetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Kilimo
Mhe.Kanali Ahmed amesema kwamba pikipiki zinawezesha maafisa ugani kuwafikia wakulima katika mashamba yao ili kutoa ushauri wa kitaalamu katika kuongeza mnyororo wa thamani na ufanisi wa kilimo kwa wakati ili kuongeza uzalishaji wa mazao
Aidha Mkuu wa Mkoa akiwa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba katika ziara yake ya siku moja ametembelea mashamba mawili ya mfano ya zao la Korosho na kuzungumza na wananchi wa Nanhyanga ambapo amewasistiza kuendelea na operesheni ya “Ondoa mapori ongeza Uzalishaji” kwa kuzingatia matumizi ya mbegu bora na upandaji wa kufuata ushauri wa wataalamu wa kilimo
RC akijibu kero za wananchi ambazo ziliwasilishwa na Mbunge wa Jimbo la Tandahimba Mhe.Katani Katani na Diwani wa Kata hiyo Mhe.Abbas Namaneha katika kikao hicho amewataka waendesha pikipiki (bodaboda) kuzingatia sheria za barabarani lakini pia Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama wa barabarani kusimamia sharia,haki na busara katika kutekeleza majukumu yao
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa