Na Kitengo cha Mawasiliano
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Mhe.Baisa Baisa ameongoza Mkutano wa Kwanza wa Baraza la Madiwani Robo ya Pili na kujadili taarifa za Kata ambapo katika Baraza hilo Mhe.Baisa amewasisitiza Madiwani kuendelea kuwaelimisha Wananchi umuhimu wa kuwapeleka watoto Shuleni ili wapate haki yao ya Msingi.
"Niwapongeze Madiwani kwa ziara ya kuhamasisha Wananchi kuwapeleka watoto Shuleni , tuendelee kushirikiana katika hilo, hatuna sababu ya kulalamika kuhusu Madawati wala Madarasa , Serikali Awamu ya Sita imeboresha Miundombinu ya Elimu" Mhe.Baisa
Sambamba na hilo Mhe.Baisa amewaasa Madiwani wa Halmashauri hiyo kuwapenda na kuwatunza watumishi wa Umma ili waweze kukaa kwa muda Mrefu wakiwahudumia Wananchi.
" Mkahamasishe jamii tuwashikilie walimu tulio nao kwa sababu wanatufundishia watoto wetu na tusiweke mazingira ambayo yatawafanya wafikirie kuhama, walimu wanahitajika maeneo Mengine katika Nchi hii tujitahidi kuwatunza" Mhe.Baisa.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa