Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Ndugu Said Msomoka amekabidhi vifaaa vya zaidi ya shilingi milioni 27 kwa idara na vitengo vya halmashauri ili kuboresha huduma
Mkurugenzi Mtendaji ndg Said Msomoka akikabidhi vitendea kazi kwa Idara ya Utawala
Akikabidhi vifaa hivyo ambavyo ni komputa,printa,laptop na vifaa vingine kwa idara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Utawala,Fedha,Mipango,Ujenzi,Kilimo na Ushirika,kitengo cha Tehama na ukaguzi wa ndani
Mkurugenzi Mtendaji ndg Said Msomka (kushoto)akimkabidhi Afisa Tehama Joseph Mongi Kishikwambi kwa ajili mifumo na habari
“Vifaa hivi vitunzwe ili kuendelea kuboresha utoaji wa huduma katika mazingira yetu ya kazi na kutambua kuwa fedha hizi ni nyingi hivyo umakini wa utunzaji wa mali ya umma uzingatiwe,”amesema Ndugu Msomoka
Mkurugenzi Mtendaji (kulia)akimkabidhi vitendea kazi Afisa Maendeleo Neema Shungu
Naye Mweka hazina wa Wilaya Ally Machella amesema katika idara yake vifaa hivyo ni muhimu katika ukusanyaji wa mapato kwenye maeneo mbalimbali hivyo changamoto hiyo itakuwa imepungua
Mkurugenzi Mtendaji (kushoto) akimkabidhi Mweka hazina Ally Machella vitendea kazi
“Nashukuru kwa vifaa hivi naamini huduma zetu zitaboreka na tutavotunza kwakuwa tunatambua umuhimu wa vifaa hivi katika idara yetu hususan katika ukusanyaji wa mapato katika vyanzo vyetu mbalimbali,”amesema ndg Machella
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa