Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tandahimba Ndugu Saidi Msomoka amepokea mipira 14 ,pampu na filimbi kwa ajili ya uhamasishaji wa michezo kwa wanafunzi wa shule za sekondari
Mkurugenzi Mtendaji (kulia)wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ndugu Said Msomoka akipokea mipira kutoka kwa meneja wa mradi bi,Thea Swai
Akipokea mipira hiyo ofisini kwake kutoka kwa shirika la Msaada wa Uendelezaji wa Michezo(Sports Development Aid) na kukabidhi kwa wakuu wa shule za sekondari ya Namikupa,Kitama,Milongodi,Naputa na Tandahimba amesema kuwa walimu wahakikishe wanajenga hamasa kwa wanafunzi kupenda michezo
Mkurugenzi Mtendaji ndg Said Msomoka (kushoto) akimkabidhi mipira miwili mwalimu wa sekondari ya Tandahimba(kati) Afisa Elimu Sekondari Wilaya Sosthenes Luhende akishuhudia tukio hilo
“Nawashukuru kwa vifaa hivi lakini pia walimu mtumie vizuri nafasi hii kuhamasisha michezo ili kupunguza mihemko mingine isiyofaa kwa wanafunzi,wakishiriki michezo itawajenga kiakili na kiafya ,nitapita katika maeneo ambayo mipira hii imetolewa kujiridhisha endapo michezo inafanyika,”amesema ndugu Msomoka
Picha ya pamoja Mkurugenzi ndugu Said Msomoka , meneja wa mradi na walimu wa shule tano ambao wamekabidhiwa mipira na mradi huo
Naye Meneja wa Mradi wa Empowered Girls Speaker out ambao upo chini ya shirika hilo Thea Swai amesema kuwa nia ya mradi huo ni kuhamasisha michezo nakutoa elimu ili kuwaepusha na mimba za utotoni,,utoro na ufaulu mdogo kwa shule za sekondari
Meneja wa Mradi bi Thea Swai akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji mipira
“Tunaamini michezo inaleta hamasa kwa wanafunzi hivyo tunatumia nafasi hiyo kutoa elimu za stadi za kazi, kuwajenga kiafya na kujitambua ili kuepuka mimba za utotoni,utoro na ufaulu mdogo,”amesema bi Swai
Picha ya pamoja Mkurugenzi Mtendaji,Afisa Elimu Sekondari,Meneja wakuu wa shule za sekondari na timu ya mradi huo
Vifaa ambavyo amepokea ni pamoja na mipira ya netball,football, volleyball,basketball,pampu na filimbi, shule tano kila shule mipira miwili wa netball na football
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa