Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Said Msomoka amekabidhi vifaa vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 4 kwa shule ya watoto wenye mahitaji maalum Mjimpya
Miongoni mwa vifaa ambavyo amekabidhi Mkurugenzi Mtendaji Said Msomoka
Akikabidhi vifaa hivyo ambavyo ni magodoro ,televisheni mbili na Redio shuleni hapo amesema kuwa anafahamu mahitaji ni mengi lakini atajitahidi kupunguza changamoto ambazo zimeainishhwa na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo
Mkurugenzi Mtendaji Said Msomka (katikati) akiwa pamoja maafisa Elimu (kushoto) na Mdau wa Elimu (kulia)
“Natamani msome katika mazingira mazuri zaidi kama mpo ulaya lakini rasiliamali zetu ni chache hata hivyo tutashughulikia changamoto hizi kwa msimu huu namuagiza Afisa Mipango ahakikishe tunamaliza changamoto hizi kama mabati kuvuja,ukosefu wa viti ili tuziwahi mvua ,”amesema Msomoka
Wanafunzi wakibeba magodoro hayo baada ya makabidhiano
Naye Kaimu Afisa Elimu Msingi Martha Sinkamba amesema kuwa wazazi walete watoto wenye ulemavu wa akili katika shule hiyo waweze kupewa ujuzi na elimu ili waweze kujisaidia wenyewe katika shughuli zao mbali mbali za kila siku
Mwalimu Mkuu(kushoto) akitoa shukrani kwa Kaimu Afisa Elimu Msingi Martha Sinkamba(kulia)
Naye Mdau wa Elimu Dorice Jeremiah ameweza kutoa magodoro 8 kwa ajili ya watoto hao”Mimi pia ni mzazi nimeguswa kuleta magodoro haya baada ya kupata taarifa kuwa wana uhitaji wa magodoro yaliyokuwepo ni chakavu, natoa wito kwa wananchi na wadau wengine kuwasaidia watoto wetu wenye mahitaji maalum,”amesema Jeremiah
Mdau wa Elimu Dorice Jeremiah akizungumza na wanafunzi wenye mahitaji maalum
Aidha Mwalimu Mkuu wa shule maalum Mjimpya Karim Chipuputa amesema hadi sasa shule ina wanafunzi 80 wavulana 40 na wasichana 40 hivyo ameishukuru serikali kwa vifaa hivyo na mdau ambaye ametoa magodoro 8
Mkurugenzi Mtendaji Said Msomoka(kushoto)akipokea risala kutoka kwa mwalimu mkuu Karim Chipuputa(Kulia)
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa