Na Kitengo cha Mawasiliano
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Mhe.Baisa Baisa amewataka Wazabuni kufikisha vifaa vya ujenzi kwa wakati kwenye miradi ili iweze kukamilika kwa wakati .
Ameyasema hayo Januari 8,2025 akiwa kwenye ziara ya Kamati ya Fedha Utawala na Mipango ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo kwa kipindi cha robo ya pili 2024/2025 ambapo amesema kuwa baadhi ya wazabuni huchelewesha kufikisha vifaa kwenye eneo la miradi na kusababisha baadhi ya miradi kutokamilika kwa wakati.
Miradi iliyotembelewa na Kamati ya Fedha ni Ujenzi wa Shule ya Sekondari Mkwedu na mradi wa ukamilishaji wa bweni la Mahuta Sekondari ambapo jumla ya miradi hiyo ni shilingi Milioni 613 .1
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa