Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Tandahimba Said Msomoka ametangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu kwa nafasi ya Ubunge ambapo Katani Ahamad Katani ameibuka kuwa mshindi kwa kupata kura 51051 kati ya kura 85896
Akisoma matokeo hayo amesema kuwa vyama vilivyogombea ni sita,idadi ya waliopiga kura ni 85896 kura zilizoharibika ni 9803 vyama hivyo ni CCM Katani Katani amepata kura 51051,ACT Alphonce Hitu kura 20799,Chadema Nasra Tayari 6827,CUF Makumbuli Uledi kura 4152,,ADC Hamis Hassan kura 1863,NCCR Mageuzi Mbaraka Tayari 1204
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Tandahimba Said Msomoka mara baada ya kumtangaza Mshindi
Aidha amesema kwa upande wa nafasi ya Urais katika Jimbo la Tandahimba CCM imepata kura 51175,CHADEMA kura 28915,ACT kura 2277,NCCR kura 223,ADC kura 212,CUF kura 1020,AFP kura 65,UMD kura 43,CHAUMA kura 271,UPDP kura 87,DP kura 90,MAKINI kura 110,SAU kura173,TADEA kura 406 na NRA kura 1087
Naye Mshindi kwa nafasi ya Ubunge Katani Katani amewashukuru wananchi wa Ta ndahimba kwa kumuamini kumpa nafasi hiyo na kuwaahidi kuwa atayatekeleza yale ambayo amewaahidi kwenye kampeni
Mshindi wa Ubunge Jimbo la Tandahimba Katani Ahmad Katani mara baada ya Kukabidhiwa hati ya kuchaguliwa
“Nawashukuru wana Tandahimba kwa kuniamini wameonyesha imani yao kwangu,nami nawaahidi nitakwenda kutumikia kwa uadilifu mkubwa na nitatekeleza yale ambayo nilikuwa nayaahidi wakati wa kampeni,”amesema Katani
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba naye akitekeleza haki yake ya msingi ya kupiga kura
Uchaguzi katika Jimbo la Tandahimba kwa upande wa nafasi ya Udiwani kwa Kata 32,CCM imeweza kuchukua Kata 30 ,kata moja ya imechukuliwa na ACT na Kata moja ya Miuta uchaguzi unatarajiwa kurudiwa
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa