Na Kitengo cha Mawasiliano.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Ndg.Francis Mkuti amewataka washiriki wa mafunzo ya Mfumo wa kidigitali wa ukusanyaji wa maoni ya Mama na Mwana kuzingatia mafunzo hayo ili kuboresha huduma za mama wajawazito na watoto wenye siku 28 katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba.
Akifungua mafunzo ya siku moja leo Februari 23,2024 kwenye ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ambapo washiriki ni Watoa huduma za afya ,Watendaji wa Vijiji na wahudumu wa afya ngazi ya jamii (WAJA) amesema kuwa mfumo wa utoaji mrejesho utaongeza ufanisi kwa wataalamu na kujitathimini.
" Mkazingatie mafunzo haya ili kufanikisha na kuleta matokeo mazuri ya Serikali ya kuboresha huduma kwa Mama na Mwana kwenye Halmashauri yetu,lakini mfumo huu utawezesha wataalamu kila mmoja kwenye eneo lake kujitathimini na kuwa na takwimu sahihi za mama wajawazito na watoto wa mwezi mmoja ," amesema Mkuti
Kwa upande wake Mwezeshaji Dkt..Makarioss Makarioss amesema mafunzo hayo yanalenga kuboresha huduma za mama na watoto wachanga ili kuhakikisha wakina mama wanapokwenda kupata huduma za kliniki wanatoa maoni ya huduma walizopata ambayo yatarudisha mrejesho kwa watoa huduma na kituo husika.
" Mama Mjawazito akifika kliniki ataelekezwa jinsi ya kutumia mfumo huu kwa kutumia simu yoyote ambapo atajisajili na kuaandika neno Mama kwenda namba 15077 buree na atakuwa anaulizwa huduma alizofanyiwa katika kituo alichohudhuria,mfumo huu hautaonesha jina wala namba yake,itaonesha maoni yake,hapo awali mfumo uliokuwa unatumika ni sanduku la maoni lakini ilikuwa ni naira kukuta maoni," amesema Mwezeshaji
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Mwl.Sostheness Luhende amesema washiriki wahakikishe mafunzo hayo yataleta maboresho katika huduma ya mama na Mwana kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba na kupunguza Vifo vya mama na mtoto.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa