Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Mtwara yamefanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mpapura ambapo Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe.Kanali Patrick Sawala amewaongoza Wananchi wa Mkoa huo kupokea Mwenge wa Uhuru 2024 ukitokea Mkoa wa Lindi.
Aidha, Viongozi wa Wilaya ya Tandahimba wamefika na kupokea Mwenge wa Uhuru akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Michael Mntenjele, Katibu Tawala, Mwenyekiti wa Halmashauri, Kaimu Mkurugenzi na Viongozi wengine.
KAULIMBIU: "TUNZA MAZINGIRA NA SHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA UJENZI WA TAIFA ENDELEVU "
#kaziiendelee
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa