Wajasiriamali wa biashara ya chakula maarufu Baba Lishe na Mama Lishe Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba wamepewa Elimu ya Matumizi sahihi ya nishati safi ya kupikia ili kutunza afya zao,kuokoa muda wa kupika sambamba na utunzaji wa mazingira .
Mafunzo hayo yameandaliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba kupitia Idara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji ambayo yamefanyika leo Februari 6,2025.
Akizungumza na wajasiriamali hao Mkuu wa Idara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Winifrida Robson amesema lengo la mafunzo hayo ni kutoa elimu ili kuhama kutoka kwenye matumizi ya nishati chafu za kupikia ambazo ni kuni na mkaa na kuhamia kwenye nishati safi za kupikia .
Kwa upande wake Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ASF.Elizabeth Mpondele amewasilisha mada na kuwasistiza wajasiriamali kuchukua tahadhari ya nishati hizo kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza .
Naye Meneja wa Benki ya Ushirika Tawi la Tandahimba(COOP BANK) Baraka Ondiek amewahimiza wajasiriamali hao kutumia benki hiyo ili kuwainua kiuchumi kwa kuomba mikopo yenye riba nafuu kufikia malengo yao.
#Tandahimba tumejipanga kazi zin
aendelea
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa