Na Kitengo cha Mawasiliano
Mahudhurio ya wanafunzi wa kidato cha kwanza kuripoti shule yanaendelea kuongezeka ambapo hadi kufikia leo wanafunzi asilimia 81 wameripoti shule katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba
Akitoa taarifa ya warioripoti shule kwa kidato cha kwanza Januari 25,2023 Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari Mwl.Sosthenes Luhende kwa Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amesema kuwa wanafunzi waliochaguliwa kuanza kidato cha kwanza Jumla yao ni 5,288 wavulana 2525 na wasichana 2763 ambao hadi leo walioripoti shule ni asilimia 81
Aidha amesema kuwa walioripoti shule 4107 sawa na asilimia 81,waliohamia shule za umma 176 waliohamia shule binafsi 20 na ambao hawajaripoti mpaka jana januari 24,2023 ni wanafunzi 985sawa na asilimia 102,Awali maoteo ni 7305 walioandikishwa 6953
Kwa upande wa darasa la kwanza maoteo ni 6808 walioandikishwa ni 6945 sawa na asilimia 102,awali maoteo 7305 walioandikishwa 6953
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amepongeza jitihada za viongozi ngazi ya vijiji, kata na tarafa kufanikisha wanafunzi hao kuripoti shule ambapo sasa wanafuatwa nyumba hadi nyumba “Operesheni ripoti shule”
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa