Wakuu wa Idara na vitengo pamoja na Watendaji Kata 32 wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba wamepatiwa mafunzo ya Elimu ya Uraia na Utawala bora ili kujenga uelewa wa pamoja wa haki na wajibu katika utekelezaji wa majukumu .
Mafunzo hayo yamefanyika leo Januari 31,2025 kwenye ukumbi wa Mikutano wa Mkuu wa Wilaya ambapo Mwezeshaji Ndg.Nicholous Mhagama akiwasilisha mada kwa washiriki amesema Elimu hiyo inatolewa ili kuwakumbusha kuzingatia miongozo ,sheria,taratibu na kanuni sambamba na kufanya mikutano na wananchi ili kuibua miradi ya Maendeleo.
Naye Mwezeshaji Ndg.Prosper Kisinini amesema kiongozi anatakiwa kuzingatia Misingi ya Utawala bora kwa kutoa maamuzi sahihi kwa Wakati Uadilifu,Uwazi na utoaji wa huduma kwa usawa,Ushirikishwaji,ufanisi wenye tija.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Ndg.Karimu Mputa akifunga mafunzo hayo amewahimiza Watendaji wa Kata kuzingatia miongozo kwenye utekelezaji wa majukumu yao.
Mafunzo hayo yameandaliwa na Wizara ya Sheria na Katiba.
#Tandahimba tumejipanga kazi zi
naendelea
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa