Na Kitengo cha Habari na Mawasiliao
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amefungua mafunzo ya mfumo wa ujifunzaji Kielektroniki (MUKI) kwa madiwani wa Halmnashauri ya Wilaya ya Tandahimba
Madiwani wakimsikiliza Dc Sawala (hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo
Amesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku katika maeneo yao ili wananchi waweze kupata maendeleo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Mhe.Baisa Baisa akifafanua jambo
“Madiwani katika mafunzo wawezeshaji watatoa mada mbalimbali ambazo zitawasaidia katika utekelezaji wa majukumu yenu,”amesema Dc Sawala
Aidha amesistiza madiwani kuendelea kusimamia masuala ya elimu,kilimo,ulinzi na usalama na wananchi kuendelea kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo katika maeneo yao
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Patrick Sawala akifungua mafunzo ya madiwani
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba akifunga mafunzo amesema anatumaini mafunzo hayo muhimu watayatendea kazi na kuwaahidi kuwanunulia vishikwambi(tablets) ili kuboresha utendaji kazi
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Tandahimba ndugu Mussa Gama akifunga mafunzo hayo
“Wawezeshaji wameeleza changamoto ya mtandao wakati wakitoa mafunzo ya mfumo lakini naamini kwa muda wa siku mbili mafunzo haya mtayafanyia kazi ili kuboresha utendaji kazi kwa wananchi,”amesema
Wawezeshaji wakiwasilisha mada kwa madiwani
Katika mafunzo hayo ya siku mbili ambayo yalianza Januari 24,2022 na kufungwa leo Januari 25,2022 wawezeshaji wameweza kuwasilisha mada mbalimbali ikiwemo mfumo wa ujifunzaji kielektroniki
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa