Na Kitengo Cha Mawasiliano
Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba limemuagiza Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilya ya Tandahimba Ndugu Mussa Gama kusimamia ili kuweza kupata viongozi wapya wa Mfuko wa Elimu baada ya Viongozi waliokuwepo kumaliza muda wao
Akifunga Kikao cha baraza la Madiwani cha robo ya nne Agosti 19,2023 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Mhe.Baisa Baisa amesema kuwa kwa mujibu wa sheria na taratibu kwasasa mfuko huo hauna viongozi hivyo jitihada zifanyike haraka ili kupata uongozi mpya
"Tukuagize Mkurugenzi ulisimamie ili tupate uongozi mpya wa Mfuko wa Elimu,yatolewe matangazo haraka ili watu waombe kwa nafasi ya Mwenyekiti ili mfuko uendelee kutekeleza majukumu yake,mfuko huu ni muhimu kwa maendeleo ya Elimu katika Halmashauri yetu,”amesema Mwenyekiti
Aidha madiwani wamesistiza uboreshaji wa huduma katika jengo la mionzi na ununuzi wa genereta”Tunaazimia kama baraza tutenge fedha iwe popote nje ya bajeti ili tupate chumba cha Mionzi ambacho kitafungwa Xray ya kisasa ili wananchi wapate huduma bora sambamba na ununuzi wa genereta,”amesema Mwenyekiti
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa