Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Madiwani wateule wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba wameapishwa ili kuanza rasmi shughuli za baraza la madiwani kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa Tandahimba
Tukio hilo kuapishwa kwa madiwani limefanyika jana tarehe 1/12/20202 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri na Hakimu Mkazi wa mahakama ya Wilaya ya Tandahimba Nasra Mwinshehe
Hata hivyo baada ya kuapishwa baraza la madiwani wamechagua Mwenyekiti wa Halmashauri na Makamu Mwenyekiti ambapo Mheshimiwa Baisa Abdala Baisa diwani wa kata ya Kitama (CCM) ameshinda nafasi hiyo kwa 91% na Makamu mwenyekiti Mheshimiwa Likapa Juma Nangololo diwani kata ya Mndumbwe (CCM) ameshinda kwa asilimia 93%
Katibu Tawala Wilaya ya Tandahimba Juvenile Mwambi akitangaza Mshindi Mwenyekiti na makamu
Aidha Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Alphayo Kidata akizungumza kwenye baraza la madiwani amesema kuwa wananchi wanahitaji maendeleo katika maeneo yao na madiwani ndiyo wasimamizi wa shughuli hizo
“Nawapongeza kwa kuapishwa pia nampongeza mwenyekiti na makamu mwenyekiti kwa kuchaguliwa wananchi wamewaamini mkasimamie kwa uadilifu miradi ya maendeleo kwenye maeneo yenu husika,”amesema ndugu Kidata
Naye Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Tandahimba ndugu Said Msomoka akijibu hoja mbalimbali za madiwani amesema kuwa yupo tayari kushirikiana na madiwani katika kuleta maendeleo ya Tandahimba
“Mimi nipo tayari kushirikiana na ninyi waheshimiwa madiwani ili wananchi wa Tandahimba waendelee kupata maendeleo ,”amesema ndugu Msomoka
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa