Na Kitengo cha Mawasiliano
Waheshimiwa Madiwani na baadhi ya wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi iliyopo Mkoani Morogoro wamefanya ziara ya kujifunza Mfumo wa stakabadhi Ghalani katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba
Ziara hiyo ya siku moja imefanyika Februari 28,2023 ambapo walipata taarifa kutoka kwa wataalamu wa Kilimo na Ushirika wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba jinsi mfumo huo unavyowanufaisha wakulima na kuongeza mapato ya Halmashauri
Aidha walitembelea katika Ghala la chama cha msingi Matogoro , Mitondi B na ghala kuu la Tandahimba na Newala(Tanecu) ambapo walipata taarifa ya jinsi wanavyoweza kutumia mfumo huo
Akizungumza Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Mhe.Lucas Mwamahenga amesema kwamba mafanikio ya utumiaji wa stakabadhi ghalani utawasaidia katika Halmashauri yao ili waweze kuongeza mapato na kumnufaisha mkulima
”Elimu tuliyoipata ya stakabadhi ghalani itakuwa jawabu,mfumo tunaotumia sasa hata Halmashauri inapoteza mapato lakini sasa tunakwenda kuhamasishana ili tuanze kutumia mfumo huu,”amesema Makamu Mwenyekiti
Naye Mwenyekiti wa Halmasahauri ya Wilaya ya Tandahimba Mhe.Baisa Baisa amesema kuwa mfumo huo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba umeleta manufaa kuliko mfumo wa awali ikiwa pamoja na kuongeza mapato ya Halmasahauri
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa