Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Kiasi cha zaidi ya shilingi Milioni 145 zimetumika kutengeneza meza 2492 na viti 2552 kwa ajili ya maandalizi ya wanafunzi 3653 ambao wamechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Januari 11 mwaka huu katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba
Akizungumza wakati wa kutembelea zoezi la kutengeneza samani hizo katika viwanda vidogo vidogo Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba amesema kuwa ameridhishwa na kasi ya utengenezaji wa samani hizo
Dc Waryuba (kulia) akimsikiliza Fundi (kushoto) akitoa maelezo kati ni Mkurugenzi Mtendaji Said Msomoka
“Nimetembelea ili niweze kuangalia kasi yao itatusaidia wanafunzi wetu kuvitumia viti na meza kwa wakati unaotakiwa,lakini kwakweli maendeleo ni mazuri naamini hadi kufika tarehe ya kufunguliwa shule tutakuwa tumefanikiwa katika zoezi hili naipongeza sana Halmashauri naMkurugenzi kwa jitihada wanazozifanya,”amesema Dc Waryuba
Aidha Dc aliwashauri vijana ambao wanatengeneza vifaa hivyo kutumia vifaa maalum ili kuweza kuepuka madhara mbali mbali yanayoweza kuwapata kutokana na mionzi mikali inayotokana na kuchomelea
Dc Waryuba akitoa ufafanuzi wa jambo
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tandahimba Said Msomoka ambaye alikuwa kwenye ziara hiyo amesema kuwa fedha hizo zimetolewa na mfuko wa elimu ili kufanikisha kupatikana kwa samani hizo kwa wakati muafaka
“Fedha hizi wametoa mfuko wa Elimu baada ya kutambua umuhimu wa jambo hili la maandalizi ya kidato cha kwanza, katika Halmashauri yetu tuna upungufu wa viti na mezakwa kidato cha kwanza baada ya kutembelea kwenye shule zetu za sekondari 28 zilizopo na kukuta upungufu huo,”amesema Mkurugenzi
Mkurugenzi Mtendaji ndg Msomoka (kati)akimweleza jambo Fundi (kushoto)
Kwa upande wa madarasa Mkurugenzi amesema kuwa Halmashauri kwa mwaka 2019/2020 iliweza kujenga vyumba vya madarasa zaidi ya 70 hivyo upungufu wa madarasa kwa kidato cha kwanza mwaka huu hakuna
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa